} });
 

 

Hatimaye nyota wa muziki nchini Tanzania, The African Princes ‘Nandy’ ameachia EP yake Nyimbo za Dini ‘Wanibariki’. EP hiyo ina nyimbo tano ambazo ni ‘Wanibariki’, ‘Umenifaa’, ‘Nipo Naye’, ‘Asante’ na ‘Noel Song’.

Nandy, jina halisi, Faustina Charles Mfinanga amesema alikuwa na ndoto ya kutoa kazi yenye Nyimbo za Dini siku moja kwa sababu amekuwa mpenzi mkubwa wa nyimbo hizo tangu akiwa mtoto hivyo, kwa kufanikiwa kuachia EP hii ya ‘Wanibariki’ ametimiza ndoto zake.

“Tangu nikiwa mdogo nimekuwa sana nikimpenda sana Mungu, mimi ni muumini mzuri sana wa kanisani na kitendo cha kutoa EP hii (Wanibariki), nimetimiza ndoto zangu,” Nandy.

‘Wanibariki EP’ imetayarishwa kwenye studio za Wanene kwa ushirikiano wa karibu na kampuni ya Boomplay na Nandy mwenyewe.

Mbali na EP hii, Nandy amewahi kufanya ‘cover’ za nyimbo za dini za waimbaji kama Joel Lwaga (Mimi Ni Wa Juu) pamoja na Angel Benard (Nikumbushe Wema Wako).soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top