
Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu baada
ya kukutwa na hatia ya usadi na kueneza ushawishi.
Hukumu hiyo iliyotolewa na mahakama mjini Paris inajumuisha mwaka mmoja gerezani na
miaka miwili ya kifungo cha nje.
Bwana Sakorzy alikuwa anashtakiwa kwa kujaribu kupata taarifa za ndani kinyume cha sheria
kuhusu uchunguzi juu ya ufadhili wa kampeni zake kutoka kwa jaji mwaka 2014.
Mahakama hiyo imesema Sarkozy atakuwa na haki ya kuomba kuzuiliwa nyumbani kwa
kutumia bangili ya umeme.
Washtakiwa wenzake wawili ambao ni wakili Thiery Herzog na jaji Gilbert Azibert, pia
wamekutwa na hatia na wamehukumiwa kifungo sawa na chake.
Baadae mwezi huu, Sarkozy atakabiliwa na kesi nyingine pamoja na watu wengine 13 kwa
mashtaka ya kufadhili kinyume cha sheria kampeni yake ya urais mwaka 2012.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment