} });
 

 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilimu amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio la Mgonjwa, Piche Mkuja anayedaiwa kumshambulia kwa Kisu, Muuguzi wa Kituo Cha Kuhudumia Wagonjwa wa Ukoma Nazareti, Ifakara Wilaya ya Kilombero Agatha John (50),

Kamanda Musilimu amesema tukio hilo limetokea March 5, mwaka huu wakati mgonjwa huyo alipofika katika hospitali hiyo kwa lengo la kupatiwa matibabu.

Amesema muuguzi ambaye ni marehemu alifika katika eneo alikolazwa mgonjwa huyo l ili kukagua maendeleo yake ndipo baada ya kufika karibu, mgonjwa huyo alichomoa Kisu na kumchoma muuguzi tumboni kisha naye kujichoma sehemu za tumboni kwa lengo la kutaka kujiua .

Musilimu amesema baada ya tukio hilo wafanyakzi wezake walimchukua muuguzi huyo na kumpeleka Hospitali ya St.Francis ili kupatiwa matibabu ambapo muda mchache badae alifariki

Hadi sasa upelelezi unaendelea kwani mara baada ya tukio muuguzi alifariki muda mchache badae mtuhumiwa nae akajichoma tumboni kwa lengo la kutaka kujiua na sasa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya st. Francis chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi na hali yake inaendelea vizuri lakin taarifa za awali zinaonesha kuwa mtuhumiwa hana tatizo la afya ya akili” amesema.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top