} });
 

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 19 Machi, 2021 ataapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Haa ya kuapishwa kwake itafanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Mhe. Samia Suluhu Hassan anaapishwa kushika wadhifa huo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kilichotokea tarehe 17 Machi, 2021.

Baada ya kuapishwa kwake, Mhe. Samia Suluhu Hassan atazungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari na kisha ataongoza kikao cha Baraza la Mawaziri.

Sikiliza Divine Radio FM 93.3MHz ili ufuatilie tukio zima.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top