} });
 

 

Serikali imesema inaendelea na jitihada za kuyakabili maambukizi mapya ya COVID-19 kwa kutafuta tiba mbadala na kusema licha ya kutumia njia za asili, inaukabili ugonjwa huo kisayansi pia.

 

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema wameshanunua mashine mbili zenye thamani ya bilioni 4 ambazo zina uwezo wa kupima kiufanisi Virusi vya Corona na zipo katika Hospitali ya Rufaa Bugando – Mwanza kwa ajili ya upimaji Kanda ya Ziwa.

 

Dkt. Mollel amesema anashangazwa na Watu wanaodhani hakuna linalofanywa na Serikali katika kukabili ugonjwa huo. Asema Serikali inatumia njia zote za kisayansi na asili, inatambua Corona inapaswa kudhibitiwa na Serikali imekuwa makini zaidi kuikabili.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top