} });
 

 

Mahojiano yaliyosubiriwa kwa hamu ya Duke na Duchess wa Sussex waliyoyafanya na Oprah Winfrey yametangazwa katika vyombo vya habari vya Marekani- huku wawili hao wakiushirikisha umma hadithi ya maisha yao katika familia ya kifalme ya Uingereza.

Wawili hao walizungumzia juu ya mahusiano yao na ufalme, ubaguzi wa rangi na matatizo ya afya ya akili yaliyowapata.

Meghan alizungumza na Oprah kwa sehemu kubwa ya mazungumzo, kabla ya kujiunga na Mwanamfalme Harry.

Hakuhiano hayo yatapeperushwa kwenye televisheni ya ITV nchini Uingereza Jumatatu usiku saa za usiku.

1. 'Mazungumzo kuhusu jinsi 'mtoto mchanga' wa Meghan' anavyoweza kuwa mweusi

Miongoni mwa madai makubwa kutoka katika mahojiano hayo lilikuwa ni suala la "mazungumzo kadhaa " na Familia ya Kifalme kuhusu jinsi mtoto mchanga wa Meghan na Harry atakavyokuwa mweusi.

"Katika miezi hiyo ambayo nilikuwa mjamzito [kulikuwa] na wasiwasi na mazungumzo kuhusu jinsi ngozi ya mtoto wangu anavyoweza kuwa mweusi atakapozaliwa," alisema Meghan.

Alisema kuwa mazungumzo yalikuwa na Harry, ambaye aliyafikisha kwangu. Wote wawili Harry na Meghan walikataa kumtaja mtu aliyesema maneno hayo katika Ufalme.

"Mazungumzo hayo, sitawahi kushirikisha Umma ni nani aliyeyasema ," alisema Harry. "Wakati mwingine yalikuwa ni magumu, yalikuwa yakutisha ."

Harry pia alisema kuwa inamuumiza kwamba familia yake haikuwahi kamwe kuzungumzia kuhusu "ubaguzi wa rangi wa ukoloni" wa vichwa vya habari na makala.

2. Kate 'alimfanya Meghan alie' - si vinginevyo

Taarifa moja ambayo ilisambaa kwenye magazeti miaka michache iliyopita ilikuwa ni kwamba (Kate mkewe Mwanamfalme William) au Duchess of Cambridge aliachwa akilia na Meghan siku moja kabla ya harusi katika mzozo juu ya magauni waliyotakiwa kuvaa watoto wa kike wasikindikizaji wa harusi.

Lakini Meghan alimwambia Oprah ukweli ni kwamba yeye ndiye aliyelizwa na Kate.

"Siku chahche kabla ya harusi [Kate] alikasirika juu ya magauni waliyopangiwa kuvaa wasindikizaji wa harusi wasichana na ilinifanya nilie ," Meghan alisema. Alisema baadaye Kate aliomba msamaha na akaleta maua na ujumbe wa maandishi wa kufanya mabadiliko.

"Sitashirikisha Umma kipande kile kumuhusu Kate itakuwa ni kumdharau ," Meghan alisema. Alisema Kate alikuwa "mtu mzuri " na alinatumai kwamba alitaka hadithi za uongo zisahihishwe.

3. Meghan alisema kuwa alikaribia kujiua lakini alinyimwa msaada

Meghan alizungumzia kuhusu jinsi alivyokua mpweke baada ya kujiunga na Familia ya ufalme na kupoteza uhuru wake. "Nilipojiunga na familia , hiyo ndio ilikuwa mara ya mwisho hadi tulipokuja hapa ndipo nilipoona pasipoti yangu, leseni yangu ya gari, , mageti yote yalifungwa," alisema.

Alisema kuwa afya yake ya akili ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba "sikutaka kuishi tena ".

" Nilikwenda katika taasisi na nikasema ninataka kwenda mahali fulani kupata usaidizi, nikasema sijawahi kujihisi vile kabla na nilihitaji kwenda mahali, fulani, na nikaambiwa siwezi, kwamba hilo lisingekuwa jambo zuri kwa taasisi ."

Alisema alikwenda kumuona "mmoja wa watu wa ngazi ya juu zaidi " katika taasisi ya Ufalme na pia idara ya wafanyakazi ya Ufalme . ''Hakuna chochote kilichofanyika ,"aliongeza.

4. Meghan alizungummza na mmoja wa marafiki wa Diana

Jina la Princess Diana lilijitokeza mara kwa mara katika kipindi chotehuku wakielezea jinsi uzoefu wao ulivyofanana na ule wa Diana katika maisha yao ndani ya Familia ya Kifalme.

"Sikujua hata nizungumze na nani ," alisema Meghan, wakati wa shida . "Miongoni mwa watu niliozungumza nao ambaye ameendelea kuwa rafiki na msiri wangu alikuwa ni mmoja wa marafiki wa mama yake na mume wangu.

"Kwasababu ni nani mwingine ambaye angeelewa maisha yakoje mle ndani ya Ufalme ?"

5. Harry anahisi 'aliangushwa' na baba yake Charles

Oprah alimuuliza Harry kuhusu uhusiano wake na familia yake na hasa baba yake Mwanamfalme wa Wales, na kaka yake Prince William -the Duke of Cambridge.

Wakati mmoja baada ya kujiondoa katika majukumu ya afisa wa ngazi ya juu ya Ufalme, Harry alisema Charles "aliacha kupokea siku zangu".

"Ninahisi niliangushwa kwasababu ameishawahi kupitia hali sawa na yangu, anafahamu maumifu yalivyona Archie ni mjukuu wake.

"Lakini wakati huohuo, bila shaka nitampenda daima lakini kuna maumivu ambayo yametokea na nitaendelea kujaribu kuponya huo uhusiano wetu kama moja ya vipaumbele vyangu ."

Kuhusu kaka yake William, Harry alisema kuwa anampenda sana na wamepitia matatizo makubwa pamoja maishani mwao. "Lakini tumekuwa katika mwelekeo tofauti kimaisha ."

6. Lakini uhusiano kati ya Meghan na Harry na Malkia ni mzuri

Harry alisema ana uhusiano "mzuri sana" na bibi yake (nyanya) na amezungumza nae zaidi katika kipindi cha mwaka uliopita-ikiwa ni pamoja na simu za video na Archie -kuliko alivyowahi kuzungumza nae kwa miaka mingi.

"Ni Kanali wangu mkuu , sawa? Ataendelea daima kuwa hivyo."

Meghan pia alimsifu Malkia na alisema kuwa aliwapatia yeye na mume wake vipuli vizuri sana wakati walipochumbiana kwa mara ya kwanza pamoja na kujifunika naye blanketi ili kujikinga baridi waliposafiri naye.

7. Harry 'alijitenga rasmi'

Katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2020, Harry alisema familia yake "imenitenga kabisa kifedha ".

Alisema mikataba ya Netflix na Spotify ambayo yeye Meghan waliipata ya kufanya vipindi na Meghan (podcasts) havikua sehemu ya mpango lakini "Ilinibidi nipate usalama kwa ajili yetu ".

"Lakini nina kile ambacho mama yangu aliniachiana bila hicho tusingeweza kufanya hili ."

Wawili hao walifichua kuwa, baada ya kunyimwa fedha na Ufalme, bilionea wa Kimarekani na Mmiliki wa mkubwa wa vyombo vya habari Tyler Perry aliwapatia Harry na Meghan nyumba ya kuishi pamoja na usalama mwaka jana walipohama kutoka Canada na kwenda kusini mwa California.

8.Ukweli kuhusu picha

Meghan alisema kuwa jioni ile baada ya kumwambia Harry kwamba anahisi kujiua, walilazimika kuhudhuria tukio rasmi katika ukumbi wa Kifalme-Royal Albert Hall.

Meghan alizungumzia kuhusu picha ambayo amekua akiijutia kutokana na kumbukumbu iliyomuachia.

Alisema kuwa rafiki yake aliandika jinsi wawili hao wanavyopendeza pamoja lakini akaongeza : "Picha ile, ukiivuta kwa karibu(zoom in) kile ninachokiona ni jinsi gani vidole vyake vilivyokua vimeukumbatia mkono wangu kwa nguvu zote," alimwambia Oprah, huku akijawa na hisia za huzuni. "Tunatabasamu na kufanya kazi yetu lakini sote tunajaribu kuvumilia . "Kila wakati zile taa za Ufalme zilipozimwa nilikuwa ninaaangua kilio."

9. Meghan 'hakujfanya utafiti wowote' juu ya Familia ya Ufalme

Akizungumzia kuhusu mara ya kwanza alipokutana na Malkia, Meghan alisema kuwa alishangazwa kufahamu kuwa ilibidi apige goti.

Alisema alifikiri ilikuwa tu ''ni sehemu ya utaratibu wake" na kwamba haifanyiki ndani ya Familia ya Ufalme.

Alielezea jinsi alivyofanya mazoezi ya haraka ya kumpigia goti Malkia kabla ya ziara ya haraka ya kupata chakula cha mchana na Malkia . "Nilisema I : 'Harry ni bibi yako" alisema Meghan. "Akanijibu : 'Ni Malkia.'"

Meghan alisema kuwa hakuwa amefanya utafiti wowote kuhusu familia ya mumewe kabla ya kujiunga nayo-na akasisitiza kuwa hakuangalia mtandao wa mumewe walipokuwa wanachumbiana.

10. Walioana siku tatu kabla ya harusi yao

Mamilioni ya watu waliwatazama Harry na Meghan wakifunga pingu za maisha katika Kasri la Windsor Castle mwaka 2018.

Lakini wawili hao walifichua kuwa kiukweli ni kwamba walikuwa wamefungishwa ndoa na Askofu Mkuu wa Canterbury katika sherehe ya kawaida siku tatu kabla.

"Tulimuita Askofu mkuu na tukasema tu, 'tazama, hiki kitu, hiki ni kitu kikubwa kwa dunia, lakini tunataka ndoa yetu baina yetu... sisi tu peke yetu katika makazi yetu'."

11. Sentensi anayoipenda Archieni 'endesha salama'

Harry alizungumza kumuhusu mtoto wao wa kiume Archie, na furaha anayoipata anapokwenda kuendesha baiskeli nje pamoja nae.

Mahojiano yalijumuisha picha fupi ya video ya mtoto huyo akicheza kwenye ufukwe pamoja na na wazazi wake.

Wawili hao walitoa mzaha kwamba neno analolipenda sana kwa wiki chache zilizopita lilikuwa ni "kunywa maji", na Harry alisema kila yeyote anapoondoka nyumbani , Archie huwaambia "endesha salama".

12. Na...ni msichana

Meghan na Harry walithibitisha kuwa wanatarajia kupata mtoto wa kike katika msimu wa majira ya joto.

Harry alisema ina "furahisha sana", akiongeza kuwa: "Unaweza kuomba nini zaidi?" - lakini akasema watakua wamemaliza kuzaa baada ya mtoto wa pili kuwasili.

Wakati mahojiano yalipokuwa wakikaribia kumalizika, Oprah alimuuliza Meghan iwapo mwisho wa yote alipata maisha ya furaha aliyoyatarajia kwa kuishi na Harry . "Mazuri zaidi kuliko hadithi yoyote uliyowahi kuisoma ," alisema Meghan

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top