} });
 


Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango amerudi rasmi kazini baada ya kuugua kwa wiki kadhaa na kulazwa katika Hospitalini Dodoma……. video hii inamuonesha Ofisini kwake baada ya kurejea.

February 23,2021 alizungumza akiwa Hospitali na kueleza kuwa anaendelea vizuri “Afya yangu imeimarika vizuri kabisakabisa, Jopo letu la Madaktari wameona nina afya njema, nina uwezo wa kuanza kurudi kuendelea na shughuli za kulitumikia Taifa letu”

“Narudi kazini, kazi ndogondogo nimeshaanza za kuwatumikia Watanzania, niwaombe Watanzania tuendelee kumuomba Mungu atatuvusha, amenivusha Mimi naamini Wagonjwa wenzangu watapona”

“Nimeona niseme haya ili mjue naendelea vizuri na nimerudi kazini kwahiyo mjue kibarua wenu wa kwenda kusimamia mapato na matumizi ya Serikali, utafutaji wa mikopo na misaada na kulinda nidhamu ya matumizi ya Serikali amerudi kazini”  Waziri Dr. Mpango

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top