} });
 


Katika siku za karibuni kumeibuka matumizi yaliyokithiri ya vinywaji vya kusisimua huku wengine wakichanganya vinywaji hivyo na dawa.

 

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini watu wanaofanya shughuli kama udereva, ukondakta, wanamichezo, watu wanaofanya kazi za nguvu, wamekuwa watumiaji wakubwa wa vinywaji hivi bila kujali kiwango kinachoelekezwa na watengenezaji.

 

Kinywaji hiki ambacho ndani yake kina kemikali inayosisimua `Caffein’, kitaalamu mtu hashauriwi kutumia chupa zaidi ya mbili kwa siku hata hivyo, watumiaji wake baadhi wamekuwa wakitumia zaidi hivyo kuwa katika hatari ya kupata matatizo zaidi ya kiafya.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top