} });
 


AFISA Elimu wa Mkoa wa Lindi, Victor Kayombo amesema Wanafunzi 2,162 ambao ni sawa na 13% ya Wanafunzi 15,860 waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2021 hawajaripoti katika Shule walizopangiwa.

 

Kati ya Wanafunzi hao, Wasichana ni 1,157 na Wavulana 1,005. Kayombo ametaja Halmashauri ambazo Wanafunzi hawajaripoti ni Kilwa (481), Nachingwea (452), Mtama (390), Ruangwa (353), Liwale (292) na Lindi Manispaa (194).

 

Hata hivyo, kutokana na hali hiyo baadhi ya Wazazi na Walezi ambao watoto wao hawajaripoti wameanza kutafutwa na kuchukuliwa hatua.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top