} });
 

 

Kikosi maalum ya kupambana na ujangili katika eneo la ikolojia ya Tarangire – Manyara, kimewakamata watu wawili katika kijiji cha Moyaka wilaya ya Babati mkoani Manyara wakiuza vipande 13 vya meno ya tembo. 

 

Mkuu wa kikosi cha kuzuiwa ujangili (KDU) Kanda ya Kaskazini, Peter Mbanjoko, Februari 28 amethiitisha kukamatwa watuhumiwa hao, Benard Masalu na Yembeson Masumbuko na kupongeza kazi nzuri ambayo imefanywa na askari wa hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Burunge WMA na Chemchem ambao wamewekeza katika eneo hilo. 

 

“Nimepata taarifa za tukio hili na tayari watuhumiwa hao wanashikiliwa na jeshi la polisi na taratibu za kuwafikisha Mahakamani zinaendelea,” amesema. 

 

Mtendaji mkuu wa Taasisi Chemchem Assosiation, Walter Pallangayo amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kulitokana na taarifa za siri ambazo walizipata na wakaandaa mtego uliofanikisha kukamatwa kwao. 

 

Taasisi ya Chemchem ambayo imewekeza hoteli za kitalii na kufanya utalii wa picha katika eneo la Burunge WMA imekuwa na mfuko maalum wa kupambana na ujangili ambapo kwa mwaka Sh400 milioni zinatumika kufanya operesheni katika eneo hilo la ikolojia ya Tarangire – Manyara.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top