
Watu wasiojulikana wameshambulia Shule ya Upili ya Wasichana wilayani Jangebe na kuwateka
nyara wasichana huku wengine wakifanikiwa kutoroka huko katika jimbo la Zamfara nchini
Nigeria.
Taarifa zinaeleza kuwa wasichana hao wametekwa katika shambulizi lililofanywa na watu
wenye silaha kwenye shule ya bweni.
Mpaka sasa bado hakuna taarifa iliyotolewa na mamlaka za juu, juu ya utekaji huo.
Ikumbukwe kwamba mnamo Februari 17, watu wenye silaha walishambulia shule ya bweni
wilayani Kagara katika jimbo la Niger na kuua wanafunzi 2, kuwateka nyara wanafunzi 27,
walimu 3 na raia 15 nchini Nigeria.
Takriban watu elfu 2 wamepoteza maisha yao kutokana na mizozo katika eneo hilo, maelfu ya
watu wamelazimika kukimbia makazi yao.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment