} });
 

 

JESHI  la Polisi mkoa Kilimanjaro limemkamata na kumshikilia Peter Pius Silayo (miaka 30), mkazi wa Tegeta Dar es Salaam aliyekamatwa eneo la Kibaoni Tarakea, wilaya ya Rombo na Melchiory Prosper Shayo, (miaka 36), mkazi wa Keni wilaya ya Rombo.


Watuhumiwa hao walikamatwa kwa kosa la kimtandao kwa kusambaza taarifa za uzushi kwenye mitandao ya kijamii kinyume na sheria ya makosa ya kimtandao kuwa viongozi wakuu wa serikali kuwa ni wagonjwa.


Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa kilimanjaro Ronald Makona amethibitisha kukamatwa kwa watu hao huku akitoa wito kwa jamii na wananchi kwa ujumla kuacha kusambaza taarifa ambazo hazina ukweli, zinazoweza kusababisha taharuki kwa jamii.

 

Aidha amesema Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakaebainika kutoa au kusambaza taarifa za kupotosha umma na kusababisha taharuki kwa jamii.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top