} });
 

 

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kushusha ada za usajili wa ‘Blogs’ na ‘Online TVs’ ili vijana wajiajiri.

 

Ametoa muda wa mwezi mmoja kuhakikisha Sheria zote zimepitiwa na muda wa usajili wa mitandao hiyo umefunguliwa, ambapo awali TCRA ilitangaza kusitisha kusajili.

 

Katika hatua nyingine ameitaka Wizara yake kuharakisha Mabadiliko ya Sheria na Sera, ikiwemo mabadiliko ya Sera ya Posta huku akiwasisitiza majukumu ya Posta yalindwe.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top