} });
 


Serikali imesema  katika mwaka 2020  jumla ya vifaranga 21,676,187 vya samaki vimezalishwa kutoka katika vituo vya serikali na vya  binafsi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema vituo binafsi vimezalisha samaki 17,529,347 na vituo vya Serikali vimezalisha samaki  4,146,840 ikilinganishwa na vifaranga 17,301,076 vilivyozalishwa mwaka 2019 sawa na ongezeko la asilimia 25.3.

Ndaki amesema lengo la serikali ni kuzalisha vifaranga milioni 30 mwaka huu ambapo Vituo na Taasisi za Serikali vitazalisha vifaranga milioni nane  na sekta binafsi kuzalisha vifaranga milioni 22.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top