} });
 


KAMPUNI ya muziki ya Apple imezindua kampeni yake inayokwenda kwa jina la Spirits Rejoice, yenye lengo la kusherehekea kazi za mastaa wa Muziki wa Injili Afrika.

Kati ya wasanii waliopo katika mpango huo ni pamoja na mastaa wa nchini Afrika Kusini, Joyous Celebration – Ntokozo Mbambo, Hle na Dr. Tumi.

 

Mbali na hao, wapo wasanii wenye majina makubwa kutoka nchini Nigeria; Sinach, Mercy Chinwo, Nathaniel Bassey, Tim Godfrey na Ada Ehi.


Uchaguzi wa muziki na wasanii hao, umezingatia kutafuta kuhamasisha, kuinua na kutia moyo wasanii wengi wa ndani ya Afrika na kimataifa, wakiwemo wasanii kama Fred Hammond, Kirk Franklin na Donald Lawrence.


Kama moja ya kutoa vionjo bora vya muziki wa Injili barani Afrika, waimbaji hao wamekuwa wakiimba kwa hisia wakitumia sauti zao kwa ufundi wa hali ya juu ili kuachilia baraka za kipekee kwa wasikilizaji.


Kwa miaka mingi, muziki wa Injili umeweka mizizi yake barani Afrika na mtindo wake wa kuita (uwepo wa Mungu) na kujibiwa (kupokea), unatoka katika makabila mengi ya Kiafrika.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top