} });
 

 

Mwanaume mmoja nchini Australia amehukumiwa kifungo cha miezi 10 gerezani kwa kosa la kuwadhihaki na kuwapiga picha maafisa wa polisi wakati wakiwa wanakata roho katika ajali.

 

Mwezi uliopita Richard Pusey alikutwa na hatia katika shitaka ambalo si kawaida kutokea kwa kusababisha hasira kwa umma pamoja na makosa mengine. Mwanaume huyo mwenye miaka 42-tayari alikuwa kizuizini kwa siku 300 na anakaribia kumaliza muda wake.

 

Jaji aliyemuhukumu alisema, jambo aliliolifanya lilikuwa la kikatili na halikuwa na utu kabisa. Bado familia za wahanga wa tukio hilo hawakuridhishwa na muda wa kifungo alichopewa na kuchochea hasira kubwa kwa umma.

 

Mwezi uliopita, Jaji Trevor Wraight alisema vyombo vya habari vimemtafsiri Pusey katika hali ambayo anaonekana kuwa mwanaume anayechukiwa zaidi nchini Australia.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top