Baraza la Sanaa la Taifa BASATA jana April 14, 2021 limetoa tamko kutokana na yale yanayoendelea mtandaoni kuhusu wasanii wa muziki wa Bongofleva, baada ya Harmonize kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Mwigizaji Kajala na kupelekea kuibuka mambo mengi.
Taarifa hiyo ya BASATA imeeleza juu ya kusikitishwa kwa baraza hilo kuhusu yanayoendelea kwa wasanii juu ya Lugha sizizo za stahaa, malumbano na kukashifiana huku baraza likiwataka wasanii hao ‘kuacha mara moja’.
Hata hivyo msanii Baba Levo amethibitisha kuitwa na Baraza hilo huku Harmonize amedai atawafikisha mahakamani wale wote wanaohusika kwenye kumchafua.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment