} });
 

 

Kutokana na ongezeko la bei katika Soko la Dunia na gharama za usafirishaji, bei za Mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa yanayoingia Nchini kupitia Bandari ya Dar imeongezeka.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema bei za rejareja kwa Petroli na Dizeli zimeongezeka kwa Tsh. 142 na Tsh. 85 kwa lita, na bei ya jumla kwa Tsh. 141.92 na Tsh. 84.95 kwa lita.

Mbali na Dar, ongezeko hilo la bei pia limegusa Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara ambapo bei za rejareja za Petroli na Dizeli zimeongezeka kwa Tsh. 73 na Tsh. 105 kwa lita.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top