} });
 

 

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imeeleza kuwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limepata hasara ya Sh150 bilioni katika kipindi cha miaka mitano.

 

Akizungumza Alhamisi Aprili 08, 2021 katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma CAG, Charles Kichere amesema, “Mwaka huu imetengeneza hasara ya Sh60 bilioni na kwa miaka mitano imetengeneza hasara ya takribani Sh150 bilioni.”

 

Hata hivyo, Kichere amesema wamebaini changamoto zinazotakiwa kushughulikiwa na Serikali ili kuimarisha utendaji katika shirika hilo, “Nilibaini bodi ya wakurugenzi haina mjumbe hata mmoja mwenye uzoefu kwenye mambo ya usafiri wa anga.

 

“Kwa miaka mitano ilikuwa Sh 45 bilioni na mwaka wa fedha 2019/20 imetozwa riba ya Sh12.4 bilioni. Ndege za ATCL kusafiri kwenda nje ya nchi zinaweza kukamatwa huo ni ukweli. Pia kuna changamoto ya viwanja vya ndege nchini, ndege za ATCL haziwezi kuruka usiku….”

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top