} });
 

 

UONGOZI wa Klabu ya Simba umekanusha uwezekano wa kuondoka kwa beki na nahodha wao, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na kuweka wazi kuwa nyota huyo ameandaliwa mkataba mnono wa kuendelea kusalia Msimbazi, huku Barbara Gonzalez akisema bado ni mali ya Simba.

 

Tshabalala anatarajiwa kuhitimisha muda wake wa mkataba na Simba mwishoni mwa msimu huu, ambapo taarifa za ndani zinaeleza kuwa amebakiza mwezi mmoja katika mkataba wake.


Akizungumzia sakata hilo Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Simba, Barbara Gonzalez alisema: “Tumezisikia hizo taarifa za beki na nahodha wetu Tshabalala kutaka kusajiliwa na Yanga, lakini nipende kuwaweka wazi kuwa huyo bado ni mchezaji wetu kwa kuwa ana mkataba na Simba, lakini pia uongozi una matarajio makubwa ya kumpa mkataba mpya wa kuendelea kusalia ndani ya klabu yetu,”Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Klabu ya Simba kimelithibitishia Championi Jumatano, kuwa ni kweli kuna ofa nyingi ambazo zimeanza kuwasilishwa ndani ya klabu hiyo kwa ajili ya kumtaka Tshabalala kwa kuwa mkataba wake unaelekea ukingoni.

 

“Ni kweli kumekuwepo na klabu ambazo zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili Tshabalala kwa kuwa mkataba wake kwa sasa unaelekea ukingoni, lakini nikuhakikishie kuwa mabosi wakubwa wa Simba wanalijua hilo na hawapo tayari kumuachia aondoke bure hivyo wamepanga kufanya kila linalowezekana kuhakikisha anasaini mkataba huo.

 

“Ukiachana na ukweli kwamba Tshabalala yupo katika kiwango cha juu kwa sasa, lakini pia ni nahodha msaidizi wa kikosi chetu hivyo ni mchezaji muhimu kwetu na hawezi kuondoka kirahisi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top