} });
 

 

Baada ya miaka 62, Taifa la Cuba litaamka Jumatatu bila kuwa na Kiongozi wa Nchi anayeitwa Castro. Raúl Castro anatarajiwa kuachia Madaraka kama Katibu Mkuu wa Chama, cheo kinachotajwa kuwa na nguvu kuliko cha Rais.


Raúl aliyeingia Madarakani kama Katibu Mkuu wa Chama mwaka 2008 baada Afya ya kaka yake, Fidel Castro kudhoofika. Analiacha Taifa hilo bila chakula cha kutosha na hali mbaya kiuchumi. Uchumi umeporomoka kwa 11% mwaka 2020 kutokana na athari za COVID19.

  

Licha ya kujiuzulu wadhifa wa Kiongozi Mkuu wa Cuba mwaka 2018, Raúl alikuwa na nguvu kubwa ya Madaraka kutokana na nafasi ya Chama katika kuendesha Siasa za Nchi hiyo.


soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top