
Denmark imesitisha utoaji wa chanjo ya Covid-19 ya Oxford ya AstraZeneca kutokana na ripoti
za athari ya kuganda kwa damu, ikiwa nchi ya kwanza ya Ulaya kuchukua hatua hiyo.
Hatua hii itafanya programu ya kutoa chanjo ichelewe kwa majuma kadhaa.
Shirika la Uangalizi wa dawa barani Ulaya juma lililopita lilitangaza uwepo wa uwezekano wa
athari za kuganda damu ukihusishwa na chanjo, lakini walisema hatari ya kufa kutokana na
ugonjwa wa Covid-19 ni mkubwa, pamoja na kuwepo kwa athari hizo.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment