} });
 


Kiwanda cha nyuklia nchini Iran kilipigwa na “hujuma ” siku moja baada ya kufichua kifaa kipya cha urutubishaji wa madini ya urani, amesema afisa wa ngazi ya juu wa masuala ya nyuklia nchini Iran. 

 

Ali Akbar Salehi hakusema ni nani wa kulaumiwa kwa “kitendo cha ugaidi “, kilichosababisha kukatika kwa umeme katika kituo cha nyuklia cha Natanz kilichopo kusini mwa mji wa Tehran siku ya Jumapili.

 

Vyombo vya habari vya umma vya Israel, hatahivyo, vilinukuu vyanzo vya ujasusi ambavyo vilisema yalikuwa ni matokeo ya mashambulio ya kimtandao ya Israeli. 

 

Israel bado haijatoa kauli yoyote ya moja kwa moja kuhusiana na tukio hilo. Lakini katika siku za hivi karibuni imekuwa ikichukua tahadhari za mara kwa mara kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran. 

 

Tukio la hivi karibuni linakuja huku juhudi za kidiplomasia za kufufua mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 – uliotelekezwa na Marekani chini ya utawala wa Trump katika mwaka 2018 – zikiwa zimefufuliwa. 

 

Jumamosi, rais wa Iran Hassan Rouhani alizindua matumizi ya vifaa vya kutengeneza nyuklia katika eneo la Natanz katika sherehe ambazo zilitangazwa moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa. 

 

Vifaa hivyo vinavyofahamika kama Centrifuges vilihitajika kuzalisha urani, ambayo inaweza kutumika kutengeneza mafuta ya vilipuzi pamoja na silaha za nyuklia. 

 

Uzinduzi wa vijfaa hivyo pia ulionesha uvunjaji mwingine wa nchi hiyo wa mkataba iliousaini wa mwaka 2015, ambao unairuhusu Iran kuzalisha na kutunza kiwango kidogo cha uruniam iliyorutubishwa kwa ajili ya kutengeneza mafuta kwa ajili nishati ya viwanda vya kibiashara pekee. 

 

Iran imesema nini?

Jumapili, msemaji wa Shirika udhibiti wa ishati ya Atomic nchini Iran (AEOI), Behrouz Kamalvandi, alisema “tukio” lilitokea asubuhi likihusisha mtandao wa nishati wa kituo hicho. 

 

Bw Kamalvandi hakutoa maelezo zaidi lakini aliliambia shirika la habari la Iran -Fars kwamba “hapakuwa na majeruhi wala uvujaji “. 

 

Baadae taarifa ya televisheni ya taifa iliyotolewa na mkuu wa AEOI Ali Akbar Salehi, elezea tukio hilo kama “hujuma” na “ugaidi wa nyuklia”. 

 

“Ikilaani hatua hatua mbaya ya shambulio hilo , Jamuhuri ya kiislamu ya Iran ilisisitiza juu ya haja ya jamii ya kimtaifa Shirika la kimataifa la udhibiti wa nguvu za Atomiki [IAEA] kushugulikia ugaidi huu wa kinyuklia ,” alinukuliwa akisema.

 

“Iran ina haki ya kuchukua hatua dhidi ya wahusika,” aliongeza. 

 

IAEA ilisema kuwa inatambua kuhusu taarifa za tukio lakini haikutoa kauli. Mwezi Julai mwaka jana, pia hujuma zililaumiwa kwa moto uliowaka kwenye kiwanda cha nyuklia cha Natanz, ambako shughuli za kifaa cha centrifuge kilipigwa zinaendeshwa. 

 

Je Israeli inaweza kuwa imehusika?

Televisheni ya umma ya Israeli, Kan, ilinukuu vyanzo visivyojulikana vya kiintelijensia vikisema ukosefu wa umeme katika kituo cha nyuklia ulisababishwa na harakati za kimtandao za Israeli. 

 

Gazeti la Haaretz pia lilisema tukio hilo linaweza kuwa linaweza kuchukuliwa kuwa ni shambulio la kimtandao la Israeli.

 

Ron Ben-Yishai, mchanganuzi wa masuala ya ulinzi katika wavuti wa habari wa Ynet, alisema kwamba huku Iran ikiendelea kujiimarisha kuelekea kuwa na uwezo wa silaha za nyuklia ni jambo la “busara kuchukulia kuwa tatizo … huenda halikusababishwa na ajali, bali hujuma za kimakusudi zilizolenga kupunguza kasi ya nyuklia kwa mazungumzo na Marekani juu ya kuondoa vikwazo “. 

 

Baadaye Jumapili, waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alisema “mapambano dhidi ya Iran na watetezi wake na juhudi za Iran za kujihami ni kazi kubwa “. 

 

“Hali ambayo ipo leo sio lazima ndiyo itakayokuwepo kesho,” aliongeza, bila kuitaja Iran moja kwa moja. 

 

Mkataba wa nyuklia wa Iran, unaofahamika kama mpango wa kina wa uutekelezaji-Comprehensive Plan of Action (JCPOA), umekuwa taabani tangu Donald Trump alipoiondoa Marekani kwenye mkataba huo.

 

Chini ya utawala wa Biden juhudi za kidiplomasia zimeongezwa maradufu ili kuufufua. Lakini Bw Netanyahu ameonya dhidi ya kurejeshwa kwa mkataba huo, na kutangaza wiki iliyopita kwamba hatofungwa na makubaliano mapya na Tehran. 

 

Nini kilichotokea katika mkataba?
Mkataba wa nyuklia unairuhusu Iran kuzalisha na kutunza kiwango kidogo cha madini ya uranium yaliyorutubishwa cha hadi 3.67% pekee. Urani iliyorutubishwa hadi 90% au zaidi inaweza kutumiwa kutengeneza silaha za nyuklia. 

 

Bw Trump alisema mkataba huo ulikuwa na misingi “fikra kuu za kufikirika kwamba utawala wa wauaji unataka mpango wa amani wa nyuklia tu” na akarejesha vikwazo vikali vya kiuchumi katika jaribio la kuilazimisha Iran kufanya mazungumzo ya mkataba mwingine. 

 

Iran, ambayo inasisitiza kuwa haitaki silaha za nyuklia, ilikataa kufanya hivyo na ikalipiza kisasi kwa kukiuka ahadi zake kadhaa muhimu chini ya mkataba huo.

 

Tangu wakati huo imekuwa ikiharakisha uvunjaji wa mkata huo katika jaribio la kuongeza shinikizo kwa Marekani. Ukiukaji huo ni pamoja na matumizi ya vifaa vya kurutubisha madini ya uranium, ikifuua urtubishaji wa hadi 20%, na kuongea akiba ya nyenzo za nyuklia.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top