} });
 


Kansela Angela Merkel wa Ujerumani anaunga mkono kuimarisha hatua za kudhibiti kuenea virusi vya corona nchini kote kwa kipindi kifupi. 

Msemaji wa Merkel, Ulrike Demmer amesema hatua hiyo inalenga kudhibiti ongezeko kubwa la maambukizi na kudokeza kuwa mfumo wa afya wa Ujerumani unakabiliwa na shinikizo linaloongezeka. 

Demmer aidha amesema idadi ya wagonjwa wanaolazwa katika vitanda vya wagonjwa mahututi imeongezeka kwa asilimia tano katika kipindi cha saa 24. 

Leo, Ujerumani imerekodi maambukizi mapya takriban 10,000 kote nchini, ingawa taasisi ya afya ya Robert Koch imetahadharisha takwimu halisi huenda zikawa ziko juu kwa sababu ya maambukizi kuchelewa kuripotiwa kufuatia wikendi ya sikukuu ya Pasaka. 

Merkel anatarajiwa kukutana na mawaziri wakuu wa majimbo yote 16 ya Ujerumani Jumatatu ijayo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top