} });
 

Mkuu wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita Mhe. Said Nkumba akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wa wilaya ya Bukombe yaliyotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS). 

Mkuu wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita Mhe. Said Nkumba ameeleza kufurahishwa na mafunzo yanayotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele kuhusu kanuni bora za uzalishaji,matakwa ya viwango, namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.

Mhe. Nkumba ametoa pongezi hizo leo Jumatano Aprili 28, 2021 wakati akifungua mafunzo hayo yaliyokutanisha wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele takribani 100 wa wilaya ya Bukombe.

Amesema mafunzo hayo ni njia muafaka ya kuleta tija zaidi katika juhudi za kuliletea taifa maendeleo ya haraka kulingana na fursa zilizopo hasa kwenye sekta ya viwanda,kilimo,biashara na maeneo mengine.

Ameongeza pia Mafunzo haya ni uthibitisho wa azma ya Serikali kupitia taasisi zake katika kufanikisha malengo ya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wilaya ya Bukombe, Bw. Paul Cheyo amewataka wadau wa mchele kutumia fursa ya mafunzo hayo kuongeza utaalamu katika uzalishaji na kuweza kuthibitisha ubora wa bidhaa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe, Bw. Dionis Myinga amesema wadau wa mchele wanachangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa nchi hivyo mafunzo hayo yatawasaidia kuzalisha bidhaa zilizokidhi viwango vya ubora na usalama.

Meneja wa Utafiti na Mafunzo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Hamisi Sudi Mwanasala amesema TBS inaendelea kutoa elimu kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini ili kuhakikisha kuwa wanapata elimu kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio ili kuleta ushindani na kukuza uchumi wa nchi.

Mafunzo hayo yameandaliwa na TBS na yamefanyika katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na yataendelea kwenye wilaya ya Katoro mkoani Geita na kumalizika katika wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza. 

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top