} });
 


LICHA ya kuwa na mwendo wa kobe kwenye kucheka na nyavu, mshambuliaji namba moja wa Yanga, Yacouba Songne mwenye mabao sita na pasi nne kati ya mabao 41 ya Yanga, amepitishwa na makocha wa mataifa manne kwenye kikosi cha kwanza.

 

Yanga iliyo nafasi ya pili imeongozwa na makocha wanne mpaka sasa kwa msimu wa 2020/21 kutoka mataifa manne tofauti, ambapo walianza msimu na taifa la Serbia, kisha Burundi, Tanzania na sasa ni Tunisia.Yacouba amecheza mechi 22 za ligi kati ya 27 ambazo Yanga imecheza, amekosekana kwenye mechi tano na kumfanya atumie jumla dakika 1,375.

 

Zama za Zlatko Krmpotic wa Serbia, alicheza mechi tano na kutumia jumla ya dakika 253, ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons, dk 45, Mbeya City, dk 45, Kagera Sugar, dk 55, Mtibwa Sugar, dk 18, Coastal Union, dk 90.

 

Zama za Cedric Kaze raia wa Burundi, alitumia dakika 794 katika mechi 13 alizocheza ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania, dk 63, KMC, dk 2, Biashara United, dk 8, Gwambina FC, dk 82, Simba, dk 12, Azam FC, dk 90, JKT Tanzania, dk 54, Ruvu Shooting, dk 90.

 

Mwadui, dk 66, Dodoma Jiji dk 89, Azam FC, dk 90, Coastal Union, dk 58, Ihefu, dk 90,Mbele ya Juma Mwambusi ambaye ni Mtanzania, alicheza mechi tatu na kutumia dakika 238 ilikuwa mbele ya KMC, dk 87, Biashara United, dk 83, na mbele ya Gwambina, dk 68.

 

Mechi ya kwanza ya Nassredine Nabi raia wa Tunisia ndani ya Yanga alianza kikosi cha kwanza mbele ya Azam FC na aliyeyusha dakika zote 90.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top