} });
 

Mwanamasumbwi machachari raia wa Marekani, Floyd Mayweather a.k.a ‘Money’ amethibitisha rasmi pambano lake dhidi ya Logan Paul litapigwa siku ya Jumapili ya Juni 6  huko Hard Rock Arena Miami. 


Bingwa huyo wa dunia, ‘Money’ pambano lake la mwisho ambalo linatambulika katika masumbwi ni lile la mwezi Agosti 2017 alipomkalisja mkali wa UFC, Conor McGregor raundi 10.

 

Mayweather pia alionekana kwenye pambano lisilo rasmi dhidi ya Mjapan mkali wa kickboxer na mixed martial, Tenshin Nasukawa mwezi Disemba mwaka 2018 akipigika raundi ya awali tu kwa knockout.

 

Logan Paul ni bondia ambaye amepigana pambano moja tu na pambano hilo kupoteza dhidi ya Mayweather ambaye kapigana mapambano 50 na yote ameshinda.

 

‘Money’ ni bondia mwenye mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja, anaaminika kuwa miongoni mwa wanamichezo wanao miliki mkwanja mrefu zaidi.

 

Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 44, katika mapambano 50 aliyopigana ameshinda yote, haja poteza hata moja. Inakumbukwa aliwahi kupigana na nyota wa UFC, Conor McGregor, amewahi pia kupambana na Oscar De La Hoya, Ricky Hatton, Manny Pacquiao na Canelo Alvarez ndani ya miaka yake 21 ya tasnia hiyo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top