} });
 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Gerson Msigwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa serikali.

Kabla ya uteuzi huo, nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Dk Hassan Abbas ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Awali Rais Samia amewateua makatibu wa kuu na manaibu Katibu wakuu wakiwemo  Dkt. Moses Mpogole, Prof.Riziki Shemdoe, Dkt.Laurian Ndumbaro, Tixon Nzunda, Prof.Godius Kahyarara, Emmanuel Tutuba, Sifuni Mchome, Dkt Abel Nkono Mkubi, Grace Maghembe na Adolf Ndunguru

Pia Rais Samia amemteua Dkt. Aifello Sichwale kuwa Mganga mkuu wa serikali na Dkt. Jabir Bakari Kuwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Hata hivyo Viongozi walioteuliwa hapo jana tarehe 4/04/2021 wanatarajia kuapishwa kesho tarehe 6/04/2021  Ikulu, Dar es salaam.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top