} });
 

 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul amelitaka Baraza la Kiswahili la Taifa kuongeza kasi ya kuratibu mpango wa kuwa na vituo vya kufundishia lugha ya Kiswahili kupitia balozi zetu mbalimbali nje ya nchi.

 

Pia, Gekul amelitaka BAKITA kuhakikisha linafuatilia kwa karibu na kuhakikisha kuwa maelekezo ya viongozi wa Kitaifa kuhusu kubadili sheria na kanuni mbalimbali zilizo katika lugha ya kingereza kuwa katika lugha ya kiswahili yanafanyiwa kazi kwa haraka.

 

Aidha, Mhe. Gekul ameielekeza Bodi ya Filamu Tanzania kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kukamilisha kwa wakati mfumo wa kielektroniki wa usajili wa Wasanii hapa nchini.

 

“Hakikisheni mnawasajili na kuwafikia wasanii wote nchini ili kujua idadi yao kamili na wapi walipo ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali ikiwamo mikopo na mafunzo ya kuwaongezea ujuzi,” amesema Gekul.

 

Mhe. Gekul ameyasema hayo tarehe 27/04/2021 alipokutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya BAKITA na Bodi ya Filamu Tanzania ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuzitembelea Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top