} });
 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa dira na mwelekeo wa awamu ya sita itakuwa ni  kudumisha mazuri ya awamu zilizopita,  kuyaendeleza mema yaliyopo na kuleta mengine mapya.

“Naomba nieleze Bunge hili tukufu pamoja na Watanzania kuwa dira na mwelekeo wa awamu ya sita itakuwa ni  kudumisha mazuri ya awamu zilizopita,  kuyaendeleza mema yaliyopo na kuleta mengine mapya. Kimsingi ndio dhana na maana halisi ya kauli mbiu au salamu yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kazi iendelee, tutaenzi na kuendeleza mambo yote mazuri lakini pia tutafanya mabadiliko pale itakapobidi kwa lengo la kukuza ufanisi na tija,” Rais Samia.

Ameongeza kuwa, “Nimekuja kulihutubia Bunge baada ya Nchi yetu kupita kwenye kipindi kigumu, kama inavyokumbukwa March 17 Taifa letu lilipata msiba mkubwa wa kuondokewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Magufuli,hivyo tusimame kumuombea Mpendwa wetu”.

“Kuniamini kwa Hayati Magufuli kuwa Mgombea Mwenza wake kumeniwezesha leo hii kuwa Mwanamke wa Kwanza Tanzania kushika nafasi ya Umakamu wa Rais na hatimaye sasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, niliwahi kusema na leo narudia tena kwamba Mimi na Hayati Magufuli ni kitu kimoja, kwahiyo mengi ambayo nimepanga kuyatekeleza ni yale ambayo yalielezwa na Hayati Magufuli wakati akilizindua Bunge hili”, Rais Samia.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top