} });
 

 

Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo, ameachana na mpango wake wa kuongeza muda wa kukaa madarakani kwa miaka miwili zaidi hatua ambayo kisiasa imesababisha machafuko mjini Mogadishu na kuleta mapigano ya kijamii kati ya wanajeshi wanaomuunga mkono na wale wanaompinga.

 

Katika hotuba yake kwa taifa, Rais Farmajo ametaka ufanyike uchanguzi mpya wa Rais kwa haraka na kupongeza jitihada za waziri mkuu ambaye muda mfupi uliopita alitengua utawala wa bwana Farmajo baada ya muda wake kumalizika mwezi Februari.

 

Farmajo alisema angefika bungeni siku ya Jumamosi kurejesha mpango wa Septemba 17, mwaka 2020 wa kuongeza muda wa kukaa madarakani ambao ulipitishwa na wabunge Aprili 12.

 

Makubaliano ya mwaka 2020 ni mchakato ambao unahusisha wazee wa ukoo katika kuchagua wajumbe ambao pia uchagua wabunge wa shirikisho ambao uchagua rais.

 

“Ninatamani kuthibitisha ,kama nilivyofanya miaka iliyopita , kuwa tunahakikisha kuwa uchaguzi unafanyika Somalia kwa wakati uliopangwa na amani,” alisema.

 

Rasi alisema pia kuwa vyombo vya usalama vinahakikisha usalama kwa raia unazingatiwa na kuzuia matukio yeyote ambayo yanaweza kupelekea taifa kuingia katika mapigano. Huku baadhi ya raia wakiwa wamekimbia ghasia na kumekuwa na hofu ya wanamgambo wa al-Shabaab.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top