} });
 


Rapper maarufu wa New York ambae aling’aa sana chini ya Bad Boy, Robert Ross maarufu kama ‘Black Rob’ amefariki kutokana na tatizo la figo, Mitandao ya Marekani imeripoti.

Rob amefariki akiwa na umri wa miaka 51 ikiwa ni ndani ya siku 10 tu toka Rapper mwingine wa New York Earl Simmons ‘DMX’ afariki akiwa na umri wa miaka 50.

Rob alikulia East Harlem, New York na kuanza kuwa karibu na Label ya Bad Boy ya Diddy mwanzoni mwa 1996 na kutokea kwenye featuring kama za ‘come see me’ remix ya 112, ‘love like this’ ya Faith Evans na nyingine.

Mwanzoni mwa miaka 2000 aliachia ‘whoa!’ ambayo ilikua smash hit iliyomuingiza kwenye Top 10 ya R&B/Hiphop bora za wakati huo na inatajwa kuwa solo single pekee iliyowahi kumuingiza kwenye 100 bora za chati ya Billboard. 

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top