} });
 


Naibu Rais wa Kenya, William Ruto, ametetea uamuzi wake wa kutumia chanjo ya Sputnik-V badala ya AstraZeneca kama serikali yao ilivyoelekeza.

 

Naibu Ruto amesema hakupata mualiko wakati wa harakati ya chanjo kwa maafisa wa serikali, inawezekana kuna mtu alisahau kumpa mwaliko wa tukio hilo, huku akisisitiza kuwa hamlaumu mtu yeyote.

 

“Sitaki kulaumu mtu yeyote … labda katibu alisahau kuniarifu,” amesema Ruto. Amesema licha ya kutoalikwa kwenye zoezi la chanjo, bado alikuwa na maamuzi mengine hivyo aliamua kupata chanjo ya SputnikV ambayo amedai alilipia shilingi 7,000 za Kenya.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top