} });
 

 

Mwimbaji Staa wa Kenya Willy Paul amemuomba Rais wa Nchi hiyo Uhuru Kenyatta kuondoa lockdown iliyowekwa Nchini humo kwa lengo la kupambana na ugonjwa wa covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Sehemu ya aliyoyaandika Willy ni haya “Mr. President Wakenya walikuchagua kwa matumaini ya maisha bora na sio haya wanayoyapitia sasa hivi, kama kweli wewe ni Rais wa Watu ni muda wa kuonesha hivyo sasa hivi, unatarajia Wakenya wata-survive vipi wakati ‘umefunga’ Nchi?”

“Tunataka kufanya kazi tutengeneze pesa tulishe familia zetu na tulipe bili zetu, tumechoka, bei zinapanda, gharama za maisha juu na wakati huohuo tunalipa mikopo na hatuna pesa, tafadhali fanya jambo” Willy Paul.

Toka corona ianze kuitetemesha Dunia hadi sasa Kenya ina vifo vya Watu 2463, Wagonjwa wakiwa laki moja na elfu hamsini na moja na waliopona wakiwa ni laki moja na elfu moja, vifo vya dunia nzima kwa sasa vimefikia milioni 3 na elfu moja Wagonjwa milioni 140 na waliougua wakapona ni milioni themanini.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top