} });
 

 

Jaribu kuweka taswira ya picha ya siku ya harusi yako kila kitu kimeandaliwa lakini una wasiwasi kwa sababu haujawahi kukutana na mwanaume ambaye anataka kukuoa.

Kando na hali hiyo kuonekana nadhimu, hii ni hadithi ya Janet, ambaye alikutana na mume wake Jackson siku Spesheli ya harusi yao. 

Akizungumza kwenye mahojiano na Afrimax, Janet alisema mume wake ambaye alikuwa anaishi Marekani, alimjua baada ya video yake kusambaa akisimulia namna alivyoacha ukahaba na kuokoka.

Alisema video hiyo ilimfanya kudhalilishwa hususan baada ya kuchapishwa bila ruhusa yake lakini ilimvutia mwanaume mmoja ambaye aliguswa na ushuhuda wake. 

"Aliona ushuhuda wangu na aliguswa. Alihisi kwamba tunatakiwa kuishi pamoja milele," alisema.

Alitafuta nambari zake za simu akiwa Marekani na baada ya kuzipata alimpgia na kuanza urafiki na kisha wakaishia kuwa wapenzi kisha mipango ya harusi ilianza akiwa bado ughaibuni 

Walikuwa wakizungumza kila siku na wakati mapenzi yao yalikolea na kuwa dhabiti, alimposa kupitia simu na kisha punde si punde mipango ya harusi ilianza.

Jamaa huyo hakubabaishwa na ukweli kuwa mama huyo ana watoto 10 ambao aliwazaa akiwa kahaba.

Badala ya kubabaishwa na maisha yake ya zamani, alichagua kumuoa mwanamke ambaye alikuwa anajaribu kuishi maisha mapya. 

Janet alisema alikumbana na pingamizi kutoka kwa kanisa lake kwa kumuona kama mwenye dhambi kubwa zaidi kufanya harusi lakini alikumbatiwa na kanisa lingine ambalo liliidhinisha ndoa yake Disemba 2020.

Siku ya harusi hiyo, ndege ya bwana harusi ilitua na kukutana na mke wake kwa mara ya kwanza na kisha wawili hao walibadilishana viapo vya ndoa. Baada ya kubadilishana viapo vya ndoa, wapenzi hao walikaa pamoja kwa wiki kadhaa kabla ya mwanamume huyo kurejea Marekani na kuanza mipango ya Janet kuhamia nchini humo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top