} });
 

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kuunganisha magari cha GFA kilichoko Kibaha mkoani Pwani na ametumia fursa hiyo kuwahakikishia Wawekezaji wote kwamba Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano.

”Nimeridhishwa na kufarijika kuona hali ya kazi inayofanyika kiwandani hapa, niwahakikishie kwamba Serikali itaendelea kuwaunga mkono katika uwekezaji wenu, Rais aliona kazi yenu kupitia mitandao na akanituma nije nione” MAJALIWA

Waziri Mkuu amesema hayo ndio mawazo ya Viongozi wa Tanzania tangu Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Pombe Magufu na Rais Samia Suluhu Hassan.

”Mmewekeza kwa wakati sahihi na kwenye Nchi sahihi na uwekezaji huu lazima utawaletea faida kwa sababu sera zetu za uwekezaji ni sahihi, niwahakikishie kwamba Serikali yetu imejipanga vizuri katika kuwahudumia Wawekezaji” MAJALIWA

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top