} });
 


Hospitali nyingi katika jiji la Delhi pamoja na majiji mengine mengi zimezidiwa na wagonjwa wa mlipuko wa corona, hali inayowalazimu watu kufanya mipango ya wagonjwa wao kutibiwa nyumbani.

 

Lakini hata juhudi hizo pia zimekuwa ngumu kutokana na kupanda maradufu kwa bei za mitungi ya gesi na dawa nyengine muhimu zilizomo katika mikono ya walanguzi.

 

Anshu Priya alitumia muda mrefu jana Jumapili kutafuta mtungi wa gesi wakati hali ya baba mkwe wake ikiendelea kuwa mbaya. Hakuweza kupata hospiatali ambayo ina nafasi. Baada ya kukosa gesi madukani, ikamlazimu kuingia mtaani kwa wachuuzi.

 

Alilipa rupia 50,000 (sawa na dola 670) kununua mtungi mmoja ambao kawaida huuzwa kwa rupia 6,000. Mama mkwe wake pia anapata shida ya kupumua na Anshu anahofia juu ya hali yake. Anasema hadhani kama ataweza kununua mtungi mwengine kwa walanguzi.


Tayari Uingereza imeshatuma shehena ya kwanza ya mashine za usaidizi wa kupumua kwa wagonjwa, yaani ventilator pamoja na mashine za kuchuja oksijeni kutoka kwenye hewa.

 

Shehena hiyo imeondoka Uingereza jana Jumapili na inatarajiwa kuwasili India kesho Jumanne. “Tunasimama bega kwa bega na India kama rafiki na mshirika wetu katika kipindi hiki kigumu cha mapambano ya kukabiliana na Covid-19,” ameeleza Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson katika taarifa yake.

 

Kwa upande wa Marekani, taifa hilo linaondosha marufuku ya kutuma malighafi nje ya nchi ili kuiwezesha India kutengezeza chanjo ya AstraZeneca kwa wingi.

 

“Kama ambavyo India ilituma msaada kwa Marekani wakati hospitali zetu zilipoelemewa mwanzoni mwa janga, nasi tunadhamiria kuisaidia India katika wakati huu wanaohitaji msaada,” ameeleza Rais Joe Biden.

 

Marekani pia inatarajiwa kutuma oksijen pamoja na mavazi maalumu ya kujikinga kwa wahudumu wa afya walio mstari wa mbele.

 

Ufaransa pia imesema itatuma oksijeni.

Katika jiji la Brussels, Kamisheni ya EU imesema inapanga kutuma oksijeni na madawa pia. Mkuu wa EU Bi. Ursula von der Leyen amesema kuwa jumuiya hiyo “inakusanya nguvu ili kuendana na mahitaji ya India ya msaada wa dharura.”

 

Nchi jirani ya Pakistan – ambayo ina uhusiano mgumu na India kutokana na mzozo wa mpaka – imejitolea vifaa tiba huku Waziri Mkuu wake Imran Khan akituma salamu kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter akiomba watu kupona haraka. Taasisi ya Edhi ya nchi hiyo pia imejitolea kutuma magari ya kubebea wagonjwa 50 kwa ajili ya kuyapeleka India.

 

BBC imepiga simu kwa wasambazaji kadhaa wa gesi za hospitalini na wengi wao wamekuwa wakitaja bei ambazo ni takribani mara 10 zaidi ya bei za kawaida.


Shida anazopitia Priya zimekuwa ni hali ya kawaida kwa Wahindi wengi. Hospitali katika majiji makubwa kama Noida, Lucknow, Allahabad na Indore, hazina vitanda vilivyowazi, kote huko familia za wagonjwa zinataabika kwa kujaribu kuwauguza wapendwa wao nyumbani.

 

Lakini hali ni mbaya zaidi katika mji mkuu wa Delhi wenye wato milioni 20 ambapo hakuna hata kitanda kimoja cha wagonjwa mahututi kilichokuwa wazi.

 

India imekuwa ikiripoti zaidi ya wagonjwa 300,000 kwa siku, na idadi hiyo kubwa ya wagonjwa imeuzidi uwezo wa mfumo wa matibabu nchini humo. Jana Jumapili pekee, watu 2,767 wamethibitishwa kufariki.

 

Hata familia zinazouguza wagonjwa majumbani zinapata tabu ya kupata vipimo vya damu pamoja na vipimo vya miale kama CT scan ama x-ray.

 

Maabara pia zimeelemewa na inachukua mpaka siku tatu kupata majibu ya vipimo. Hali hiyo inawaweka madktari katika wakati mgumu wa kupima hali ya maendeleo ya mgonjwa.

 

Uchelewaji huo wa vipimo, kwa mujibu wa madaktari unawaacha wagonjwa wengi zaidi hatarini. Baadhi ya wagonjwa wamegomewa kulazwa kwa kuwa hawakuwa na majibu ya kipimo cha corona.

 

Misaada yatumwa
Jumuiya ya Kimataifa inaendelea na juhudi za kuisaidia India kukabiliana na janga hilo, hususani uhaba wa oksijeni. Uingereza, Marekani na Jumuiya ya Ulaya (EU) zote zimetangaza maamuzi yake ya kuepeleka vifaa tiba nchini humo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top