} });
 


IDADI ya watu waliokufa duniani kutokana na ugonjwa wa Covid-19 imefikia milioni tatu kufikia jana, licha ya kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo ikiendelea kushika kasi.

 

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la habari la AFP, zaidi ya vifo 12,000 duniani kote viliripotiwa kila siku katika muda wa wiki moja iliyopita na kufikia vifo milioni tatu kufikia jana Aprili 17 2021.

 

Janga hilo halionyesha dalili ya kupunguza makali yake, huku watu 829,596 wakiambukizwa virusi vya corona siku ya Ijumaa pekee, idadi hiyo ikiwa ya juu zaidi kwa watu kuambukizwa kwa siku moja.

 

Hali hiyo inaonyesha jinsi janga la corona linavyoendelea kuitikisa dunia tangu kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kuripotiwa kwa mara ya kwanza nchini China mnamo Desemba 2019.

 

Zaidi ya watu milioni 139 wameambukizwa virusi vya corona duniani kote huku janga hilo likiathiri pakubwa uchumi wa ulimwengu.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top