} });
 

 

SERIKALI ya Brazil imetoa wito wanawake nchini humo kuacha kupata ujauzito angalau hadi baada ya kushuka kwa viwango vya maambukizo ya ugonjwa wa Covid-19, ikisema aina mpya ya kirusi cha Corona nchini humo kinaonekana kuathiri zaidi wanawake wajawazito.

 

Afisa wa wizara ya afya Raphael Parente amewataka wanawake iwapo inawezekana, kucheleweshe kidogo kupata   ujauzito hadi hali ya mambo itakapokuwa sawa.

 

Pendekezo hilo la kuwataka wanawake kuchelewesha kupata uja uzito linakuja wakati ambapo nchi hiyo ilipo kusini mwa bara la Amerika inaendelea kuwa moja ya kitovu cha ugonjwa wa Covid-19 duniani.

 

Idadi ya watu wanaokufa kwa ugonjwa huo nchini Brazil kwa siku ni kubwa zaidi kuliko sehemu nyengine duniani.Hospitali zimelemewa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaohitaji huduma za dharura, na kuifanya nchi hiyo kuomba msaada kutoka washirika wa kimataifa.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top