} });
 

 

Polisi huko Nyeri, nchini Kenya wanawashikilia wanawake watatu wanaodaiwa kuibia wanaume katika kumbi za starehe.

Wanawake hao wanaojulikana kwa majina Rita Okuto, Caroline Kariuki na Caroline Wanjiku walikamatwa usiku wakiwa wanazunguka nje ya muda watu wanaoruhusiwa kuwa nje baada ya Kenya kuweka “Lockdown”.

Watuhumiwa walikutwa na simu sita, tablet, tarakilishi mpakato (laptop) pamoja na vitambulisho, kadi za ATM za watu wengine pamoja na dawa zinazosadikiwa kutumika katika kuwafanya wahanga wao kusinzia kabla ya kuwaibia.

Wanaume wawili walijitokeza kushitaki katika kituo cha polisi Nyeri na kufanikiwa kupata simu zao na kusema kuwa walikuwa na wanawake hao baa.

Washitakiwa watafikishwa mahakamani Aprili 6, kwa ajili ya kusomewa mashitaka.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top