} });
 

 

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso Aprili 18, amewasimamisha kazi kupisha uchunguzi, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) Mhandisi Tamimu Katakweba, Afisa Maji Bonde la Wami Ruvu Bw. Simon Ngonyani huku akiagiza watumishi wengine waliokuwa vinara wa kueneza chuki na kuleta taharuki badala ya kufanya kazi kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

 

Waziri Aweso ameeleza kuwa Mkurugenzi wa MORUWASA pamoja na tuhuma nyingine za kiutumishi lakini alisaini mkataba wa fedha nyingi na wakandarasi bila kushirikisha Wizara na hata bila uwepo wa Katibu Mkuu kinyume na taratibu, huku Afisa wa Bonde akisimamishwa kupisha uchunguzi wa tuhuma za ukiukwaji wa maadili ya utumishi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top