} });
 

 

Ace Magashule, katibu mkuu wa chama tawala cha ANC nchini Afrika Kusini, ameJIBU hatua ya kutimuliwa kwake chamani kwa kumsimamisha kazi Rais Cyril Ramaphosa kama mkuu wa chama hicho.

"Mimi pia, kwa kuzingatia mamlaka niliyopewa kama katibu mkuu wa ANC, na kwa kutii kikamilifu maazimio ya mkutano wa chama, namsimamisha kazi kwa muda rais wa ANC, Ndugu Cyril Ramaphosa, " Bw. Magashule alinukuliwa na vyombo vya habari akisema.

Naibu katibu mkuu wa chama, Jessie Duarte, hata hivyo amesema Bw. Magashule hana mamlaka ya kumpatia rais barua ya kumsimamisha kazi na anaweza kufanya hivyo yeye binafsi bila uungwaji mkono wa chama.

Bw. Magashule amesema atakata rufaa kupinga uamuzi wa kumfuza chamani "unaokiuka katiba" - na kusisitiza atasalia katika nafasi yake hadi rufaa hiyo itakapoamuliwa.

ANC ilimtimua Bw Magashule siku ya Jumatatno na kuonya wanachama wengine wanaokabiliwa na mashtaka ya ufisadi kwamba watafuata mkondo huo endapo hawatajiuzulu ndani muda wa mwezi mmoja.

Bw. Magashule amepinga mashtaka ya ubadhirifu, ufisadi na utakatishaji fedha yanayomkabili.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top