} });
 


Idara ya uhamiaji imewasimamisha kazi Askari wake watatu kwa tuhuma za kutumia nguvu kinyume cha sheria na maadili ya kazi zao dhidi ya Mtuhumiwa wa utapeli Alex Raphael Kyai kama ilivyoonekana katika video fupi iliyosambaa.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kulaghai na kupokea fedha kutoka kwa Wateja mbalimbali ili waweze kupata pasipoti kwa haraka pia amekuwa akijitambulisha kama Mtumishi wa Taasisi nyeti ikiwemo TAKUKURU.

“Hatua ambazo Idara imechukua dhidi ya Askari, tumewasimamisha kazi kupisha uchunguzi wa tukio lenyewe lakini pia Mtuhumiwa tumemfikisha kwenye mamlaka husika ili aweze kuendelea na utaratibu mwingine kisheria” - Dr. Anna Peter Makakala, Kamishina Jenerali wa Uhamiaji.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top