} });
 


Rais wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi amesema chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona ni hiari na hakuna mtu yeyote atakayelazimishwa.

Rais Mwinyi ameyasema hayo wakati wa ziara ya kuwashukuru viongozi wa CCM wa ngazi mbalimbali katika ukumbi wa Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Amesema wananchi wasikubali kufikishwa sehemu na kuambiwa wakichanjwa wanakufa, “dunia yote watu wamekuwa wakichanjwa. Leo tumesema hivi mamlaka ya Saudi Arabia ilishasema mahujaji hawatapokelewa kama hawana chanjo, mimi kama kiongozi wa hii nchi nifanyeje niseme basi msiende?”

“Nimesema tutaleta chanjo anayetaka akachanjwe asiyetaka aache, tuwaambie watu walielewe jambo hili Serikali hailazimishi mtu na mimi binafsi nisingetaka mtu anilazimishe iwe hiari yangu nataka nitachanjwa sitaki basi, sina budi lazima nichanjwe vinginevyo siendi hija, hiyo ndio habari ya chanjo tusiwe na maneno mengi kupitiliza.” Mwinyi

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top