} });
 


KAMA hujasikia majigambo kuelekea katika mchezo wa leo Jumanne wa robo fainali wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kati ya Mwadui FC na Yanga, basi habari ikufikie kwamba, hadi muda huu kila upande umetamba kuibuka na ushindi na kutinga nusu fainali.

 

Jioni ya leo, Yanga wanakutana na Mwadui kwenye hatua hiyo utakaochezwa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

 

Yanga imetinga robo fainali baada ya kuifunga Prisons bao 1-0, huku Mwadui yenyewe ikiiondosha Coastal Union mabao 2-0.

 

Akizungumza, Katibu wa Mwadui FC, Ramadhani Kilao, alisema:

“Maandalizi yote ya kuelekea mchezo huo yapo vizuri, wachezaji wana morali ya kutosha, ili kuhakikisha tunatinga hatua inayofuata.”

 

Naye Meneja wa Mwadui, David Chakala, alisema: “Kikosi kipo salama, hakuna majeruhi hata mmoja, tunasubiria muda ufike tu ili tuingie uwanjani, hivyo Yanga wasijiamini sana maana tuna uhakika wa kuwapiga.”

 

Yanga ambao wapo Shinyanga tangu juzi Jumapili wakitokea Singida walipoweka kambi ya muda mfupi, kupitia Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Hassani Bumbuli, alibainisha kwamba wapo imara.

 

“Tayari tupo Shinyanga na tumejipanga kwa ajili ya kufanikiwa kufuzu hatua inayofuata huku malengo yakiwa ni kufika hadi fainali.

La kushukuru Mungu hatuna majeruhi wa aina yeyote, wachezaji wamejipanga kikamilifu kuona wanaleta matokeo chanya,” alisema Bumbuli.Soma ukurasa wa 16 upate uchambuzi wa mechi za hatua hii ya robo fainali ya ASFC.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top