} });
 

 

Jacqueline Ntuyabaliwe, mjane wa Reginald Mengi amesema Mumewe hakuwa na matatizo ya akili kama inavyodaiwa  na kuwataka wanaotoa  madai hayo kuacha uzushi.

Ameandika upitia ukurasa wake wa Twitter, ikiwa zimepita siku tatu tangu Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuukataa wosia uliokuwa ukidaiwa kuandikwa na Mengi ambaye alikuwa mfanyabiashara maarufu nchini ambapo pamoja na mambo mengine ikieleza kuwa haukidhi matakwa ya kisheria ili kuwa wosia halali.

Katika maelezo yake aliyoyatoa Jacqueline amesema wanaoibua uzushi huo wanaweza kusema chochote wanachojisikia na kuchukua mali zote lakini hawezi akakaa kimya na kuacha wamchafue Mengi, atasimama na kumtetea katika hilo.

“Hii ni ripoti yake ya hospitali, huu ni kweli kwa wale ambao wanataka kupata uhakika. Mume wangu hakuwa na matatizo ya kiakili.” Jacqueline

“Mnaweza mkasema chochote mnachojisikia na kuchukua kila kitu lakini kwa hili nitamtetea hadi umauti wangu utakaponifika. Daktari Kaushik Ranchod kutoka Afrika Kusini na daktari Anthony Rudd kutoka Uingereza wanaujua ukweli kuhusu hili,” Jacqueline

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top