} });
 

Na Faustine Gimu Galafoni kutoka Jijini Dodoma

Katibu wa  CCM Wilaya Kahama Emmanuel Lameck Mbamange amemwelezea mwenyekiti mpya wa CCM taifa Samia Suluhu Hassan kuwa ni kiongozi atakayekivusha salama  chama cha mapinduzi huku akiwataka watanzania kuwa na imani naye.

Katibu huyo wa CCM Wilayani Kahama alibainisha hayo hivi karibuni jijini Dodoma wakati akifanya mahojiano maalum na Divine Fm mara baada ya kufanyika mkutano maalum wa CCM wa kumchangua mwenyekiti wa mpya wa CCM Taifa Samia Suluhu Hassan  ambapo amesema ubongo wa mwanamke ni imara kama ilivyo ubongo wa mwanaume. 

“Kura zote za wajumbe wote amepata kura za ndio kwa hiyo ushindi wake ni wa asilimia mia moja, hii inaonyesha kwamba chama cha mapinduzi wajumbe wote kutoka mikoa yote tumekuwa na imani na mheshimiwa rais wetu na kumpa nafasi ya uwenyekiti wa chama cha mapinduzi kwa asilimia kubwa sana. Na nina amini hayo ni mawazo ya wanachama wote wa chama cha mapinduzi kutoka maeneo mbalimbali ambayo tumewakilisha.” Emmanuel Lameck Mbamange     

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala Flora Sagasaga alipata fursa ya kuelezea hisia zake baada ya kupata mwenyekiti  wa kwanza wa kike kupitia chama hicho ngazi ya Taifa.

"Mimi kama mjumbe wa mkutano mkuu kutoka Shinyanga, nimejifunza kwamba Chama cha Mapinduzi bado kina tanuru, lakini Chama cha mapinduzi kinafuata katiba yake, kanuni zake na ndio maana ni chama kitulivu, kimeshika hatamu na kimeshikilia Serikali kwa muda mrefu sana."

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top