} });
 


KESI ya ufisadi dhidi ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma inatarajiwa kuanza leo, baada ya kuahirishwa mara kadhaa.


Zuma, 79, alidharau ombi la kufika mbele ya tume ya uchunguzi ambayo mwenyekiti wake ni hakimu Ray Zondo.

 

Jaji amesema ukaidi wa Bwana Zuma kunaweza kusababisha kutotekelezwa kwa sheria na kwamba ataomba mahakama ya juu ya Afrika Kusini kumhukumu aliyekuwa rais kwa kosa la kuidharau mahakama kwa kitendo chake cha kukaidi wito wa kufika mahakamani.

 

Kiongozi huyo ambaye wakati mmoja aliwahi kuwa shujaa kwa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi anatarajiwa kukana mashtaka ya udanganyifu na ulaghai katika kesi ambayo ilianza na mkataba wa silaha miaka ya 1990.


Alidai kuwa mwathiriwa wa hujuma za kisiasa- na kwamba mahakama nchini humo zinashirikiana na mahasimu wake wa kisiasa.


 Zuma pia anakabiliwa na madai mapya ya ufisadi na huenda akafungwa jela kwa kukiuka amri ya mahakama katika kesi nyingine tofauti.

 

Bwana Zuma alilazimishwa kujiuzulu kama rais mwaka 2018 baada ya kukabiliwa na madai ya ufisadi katika kipindi chote cha miaka 9 ambayo alikuwa madarakani.

 

Mrithi wake, Cyril Ramaphosa, aliingia madarakani kwa kuahidi kutatua tatizo hilo, raia wa Afrika Kusini wanaamini kesi hiyo inaweza kuashiria mabadiliko ya nchi hiyo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top