} });
 


Marekani inapania kupeleka dawa za kupunguza makali ya Ukimwi ambazo zimekwama katika bandari ya Kenya katika nchi zingine zinazohitaji, ubalozi wake nchini Kenya umesema.

Dawa hizo ziliwasili nchini Kenya mwezi Januari na zimekwama katika bandari ya Mombasa kutokana na mzozo unaoendelea wa kodi na vibali.

Ubalozi wa Marekani umesema unahofia muda wa mwisho wa matumizi ya dawa hizo,na huenda ikawa rahisi kupeleka dawa hizo katika nchi nyingine kutumika.

Serikali ya Kenya iliondolea ushuru dawa hizo lakini afisa wa mamlaka uya ukusanyaji kodi amenukuliwa na gazeti la Daily Nation akisema kwambabaadhi ya makontena bado zinasubiri kibali kutoka kwa shiriki la dawa.

Afisa kutoka shirika la madawa anasema kibali kipya kinahitajika kuombwakwani ya awali inasema mpokeaji ni Shirika la Kenya la usambazaji madawa.

Mfadhili, USAid,imepatia kampuni ya kibinafsi kusambaza dawa hiyo wakati serikali inataka shirika lake la usamazaji dawa kusimamia mpango huo.

Zaidi ya watu milioni 1.5 wanaoishi na virusi HIV wanahitaji dawa hizo na zimekuwa zikitolewa kwa mgao katika vituo vya afya ili kikidhi mahitaji hayo kwa muda.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top