} });
 


JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union ya Tanga amesema kuwa kuhusu kufukuzwa ndani ya timu hiyo anasikia tu kama wengine na yeye bado yupo kazini.

 

Mgunda amekiongoza kikosi cha Coastal Union kwenye jumla ya mechi 28, alishinda 8 moja ilikuwa mbele ya Yanga kwa kuitungua mabao 2-1, sare 9 na kupoteza 11 huku kikosi kikiwa nafasi ya 11.

 

Hivi karibuni zilienea taarifa za Mgunda kafutwa kazi ndani ya Coastal Union ikiwa ni muda mfupi baada ya kuiongoza timu hiyo kutolewa hatua ya 16 bora na Mwadui FC katika Kombe la Shirikisho.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Mgunda alisema kuwa habari hizo amekuwa akisikia kama ambavyo wengine wanaziskia.

 

“Bado ninaendelea kuripoti kazini ingekuwa hivyo hata kazini nisingekwenda, ukweli ni kwamba hata mimi hizo taarifa ninaskia kama ambavyo wanaskia wengine, hivyo kwa kuwa ninaripoti kazini basi kila mmoja anapaswa achuje mwenyewe atafute ukweli.

 

“Kwa sasa baada ya kuondolewa kwenye Kombe la Shirikisho akili zetu ni kwenye mechi zetu za ligi huko tutapambana ili kufanya vizuri,” alisema Mgunda.

 

Mchezo wake ujao wa ligi ni dhidi ya Simba unatarajiwa kuchezwa Mei 11, Uwanja wa Mkapa, ule wa mzunguko wa kwanza walipokutana ubao ulisoma Coastal Union 0-7 Simba.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top